Wanusurika wawasili Addis Ababa
19 Januari 2012Matangazo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle amesema, Wajerumani ni miongoni mwa watu hao walio salama. Watalii 5 wa kigeni, waliuawa katika shambulio lililofanywa kaskazini ya Ethiopia mapema jumanne . Miongoni mwao ni raia 2 wa Ujerumani, 2 kutoka Hungary na mmoja ni raia wa Austria.
Watu 4 wengine wametekwa nyara na haijulikani walikopelekwa. Miongoni mwao ni Wajerumani 2. Wizara ya nje ya Ujerumani imesema, inachunguza tukio hilo. Kwa mujibu wa serikali ya Ethiopia, washambuliaji hao waliokuwa na bunduki, walivuka mpaka wakitokea nchi jirani Eritrea.