1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waokoaji hawajafanikiwa kupata manusura zaidi India

3 Juni 2023

Mamlaka nchini India zimesema, waokoaji hawajafanikiwa kuwapata watu wengine walionusurika kwenye ajali iliyohusisha treni mbili za abiria na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 280.

Indien Zugunglück in Neu-Delhi
Picha: Rafiq Maqbool/AP Photo/picture alliance

Mamia ya watu wamejeruhiwa kwenye ajali hiyo inayotajwa kuwa mbaya zaidi kuwahi kutokea ndani ya miongo kadhaa.

Treni hizo ni Coromandel Express iliyokuwa ikisafiri kutoka Howrah, jimbo la Bengali magharibi kuelekea Chena, jimboni Tamil Nadu, na Howrah Superfast Express iliyokuwa ikisafiri kutoka Bengaluru huko Karnataka kuelekea Howrah.
Mkurugenzi wa kitengo cha dharura na zimamoto wa jimbo la Odisha, Sudhanshu Sarangi, amesema kufikia majira ya saa nne usiku, walifanikiwa kuwaokoa watu walionusurika na baada ya hapo shughuli iliyofuata ilikuwa ya kuitoa miili ya watu waliokufa kwenye ajali hiyo.
Waziri Mkuu wa India Narendra Mordi alikutana na maafisa mjini New Delhi alipoelezea kushtushwa na ajali hiyo na kisha alisafiri kuelekea Odisha kwa lengo la kutembelea eneo la tukio na kufika kwenye hospitali wanakotibiwa majeruhi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW