1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waokoaji waendelea kuwatowa watu kwenye vifusi Dar es Salaam

17 Novemba 2024

Vikosi vya uokozi vinaendelea kushirikiana na raia kuwasaka manusura wa ajali ya kuporomoka kwa jengo katikati ya jiji kuu la kiuchumi la Tanzania, Dar es Salaam, huku miili zaidi ikipatikana.

Afrika  Kariakoo Dar es Salaam
Waokoaji wakiendelea kuwatoa manusura wa ajali ya jengo jijini Dar es Salaam.Picha: Yakub Talib/DW

Kwa siku ya pili mfululizo, waokoaji katika taifa hilo la Afrika Mashariki wamekuwa wakichimba kwenye kifusi cha jengo lililoporomoka jana Jumamosi, wakitarajia kuwapata manusura zaidi waliokwama chini.

Jengo hilo la ghorofa nne lilianguka majira ya saa 3:00 asubuhi katika mtaa wenye shughuli nyingi wa Kariakoo, kitovu kabisa pa shughuli za kibiashara kwenye jiji hilo la bandari. 

Soma zaidi: Miili zaidi yapatikana ajali ya jengo Dar es Salaam

Kufikia mchana wa Jumapili, idadi ya waliothibitishwa kupoteza maisha walikuwa watano, huku wengine 70 wakiwa wameokolewa wakiwa hai, kwa mujibu wa kikosi cha zimamoto.

Ukiwa mmojawapo wa miji inayokuwa kwa kasi, Dar es Salaam imekuwa sehemu inayoshuhudia kupanda kwa ujenzi wa majengo ya anasa na ya kibiashara, lakini mara nyingi unaoikuka kanuni za majengo salama.

Mnamo mwaka 2016, jengo la ghorofa 16 liliporomoka kwenye mji huo na kuuwa watu 34.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW