MigogoroMamlaka ya Palestina
Wapalestina 17 wauawa kufuatia shambulio la Israel Gaza
1 Januari 2025Matangazo
Hayo yameripotiwa na shirika rasmi la habari la mamlaka ya Palestina, WAFA.
Jeshi la Israel IDF hata hivyo halijazungumzia juu ya shambulio hilo japo kupitia mtandao wa kijamii wa X, msemaji wake aliwaonya wakaazi wa al-Bureij kuondoka kutokana na uwezekano wa Israel kulishambulia eneo hilo ili kulenga wanamgambo waliokuwa wakifyetua roketi kutoka eneo hilo.
Soma pia: Wanajeshi wa Israel wavamia na kuchoma hospitali Gaza
Jeshi hilo la IDF limesema limemuua usiku wa kuamkia leo Abd al-Hadi Sabah, mwanachama wa Hamas aliyesaidia kuongoza uvamizi katika ardhi ya Israel wakati wa shambulio la Oktoba 7, mwaka 2023 lililofanywa na wanamgambo wa Hamas.