1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapalestina waandamana kumuunga mkono Rais Abbas

11 Februari 2020

Maelfu ya Wapalestina leo hii wameandamana katika eneo la Ukingo wa Magharibi, kuipinga jitihada ya Rais wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati.

Gazastreifen Gaza City | Protest gegen Friedensplan Trump & Netanjahu
Picha: Imago Images/ZUMA Press

Wakati hayo yakiendelea Rais wa Palestina Mahmoud Abbas baadae leo anatarajiwa kutoa hutoba yake kwa Umoja wa Mataifa, lakini mataifa wanachama hawatapata fursa ya kulipigia kura azimio husika. Mamlaka ya Palestina imelikataa azimio hilo na kujitoa, lakini wanadiplomasia wanasema mataifa mengi wanachama, yakiwemo ya Umoja wa Ulaya, yamepinga lugha iliyotumika katika rasimu ya azamio hilo.

Mpango wa Trump kwa Mashariki ya Kati, ambao aliutangaza Januari 28 katika Ikulu ya Marekani, umejiegemeza sana kwa upande wa Israel kwa karibu maswala yote yenye utata katika vita iliyodumu kwa miongo kadhaa. Unaonekana wenye kutoa upendeleo kwa Israel kujinyakulia sehemu kubwa ya Ukingo wa Magharibi, pamoja  na makazi ya Wayahudi ambayo ni makazi ya idadi kubwa ya watu ambao sehemu kubwa ya jumuiya ya kimataifa inawachukulia kama wakazi haramu.

Kwa sasa Palestina ambayo iliuvunja kabisa uhusiano wake na Marekani, 2017 baada ya Trump kuitambua Jerusaleem kama mji mkuu, imeutupilia mbali mpango huo. Katika maandamano haya ya leo idadi ya waandamanaji waliokusanyika katika uwanja wa Al Manara mjini Ramallah, huko Ukingo wa Magharibi, eneo ambalo ndio makao makuu ya Mamlaka ya Palestina, wameonekana wakipeperusha bendera za Palestina pamoja na mabango ambayo yamebeba ujumbe wa kulaani mpango wa Trump.

Ujumbe wa waandamanaji kuhusu Trump

Rais Donald Trump wa MarekaniPicha: Reuters/J. Roberts

Bango moja kwa mfano lililoandikwa kwa lugha ya Kiingereza limebeba ujumbe usemao "Trump ni sehemu ya tatizo, na sio suluhisho. Na lingine linalolaani limeandikwa "ni wizi wa karne" maafisa kutoka mataifa ya kiarabu wanautaja mpango huo wa Trump kama "mpango wa fedhea".

Akizungumza mbele ya umma wa waandamaji Waziri Mkuu wa Palestina Mohammed Shtayyeh alisema watu wote wa Palestina na makundi yote hasimu, taifa na waislamu wapo pamoja na Rais Mahmoud Abbas. Aliongeza kusema hali ya kufurika watu kwa mitaa yote ndio inaonesha majibu ya Waplestina kwa Trump.

Rais Abbas anajaribu kutafuta uungwaji mkono wa kimataifa dhidi ya mpoango wa Trump, huku akiwa na matumaini ya kufanikiwa ya kiasi. Umoja wa nchi za Kiarabu kwa pamoja  zimeunga mkono Palestin dhidi ya mpango huo, lakini washirika muhimu wa Marekani kama Misri na wameunga mkono jitihada za Trump na kutaka kuanza upya kwa mazungumzo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW