1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapalestina waendelea kuyakimbia mashambulizi ya Israel Gaza

9 Julai 2024

Wapalestina wameendelea kukimbia vita vikali katika mji wa Gaza City, wakati wanajeshi wa Israel wakitanuwa orodha ya maeneo wanakowataka waondoke kufuatia mashambulio.

Wapelestina wakiwa wakikimbia mashambulizi ya Israel.
Wapelestina wakiwa wakikimbia mashambulizi ya Israel.Picha: Bashar Taleb/AFP

Vikosi vya Israel vimesogea zaidi katika mji huo mkubwa kabisa wa Ukanda wa Gaza kuwatafuta wanamgambo waliojipanga upya katika eneo hilo.

Wanamgambo wa kundi la Hamas wameonya kwamba mashambulizi hayo mapya ya Israel pamoja na  watu kukimbia makaazi, ni hatua inayoweza kusababisha kuvunjika kwa mazungumzo ya muda mrefu ya kutafuta usitishaji mapigano,pamoja na kuachiliwa kwa mateka.

Soma pia:Netanyahu kupeleka wawakilishi majadiliano ya kusitisha vita Gaza

Katika siku za hivi karibuni wapatanishi wameongeza juhudi za kumaliza vita hivyo vya miezi tisa,huku ikielezwa kwamba pande zote mbili zilikuwa zikikaribia kumaliza mkwamo.

Israel iliwataka Wapalestina waondoke Gaza City kabla ya kuanza mashambulio yao jana lakini Wapalestina wamesema hakuna mahala salama.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW