SiasaMamlaka ya Palestina
Wapalestina wakalia kiti cha "Dola ya Palestina" ndani ya UM
11 Septemba 2024Matangazo
Balozi wa Palestina kwenye Umoja wa Mataifa Riyad Mansour aliketi kwenye kiti ndani ya ukumbi wa mikutano kilichoandikwa "Dola ya Palestina" ambacho kimewekwa katikati ya mataifa mawili ya Sri Lanka na Sudan.
Hatua hiyo inafuatia kura iliyopigwa na Baraza Kuu mnamo mwezi Mei ambapo idadi kubwa ya nchi wanachama ziliridhia Palestina itambuliwe kuwa mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa.
Hata hivyo uamuzi huo ulizuiwa kwa kura ya turufu ya Marekani ulipofikishwa mbele Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Licha ya hayo, azimio hilo la mwezi Mei limetoa haki zaidi kwa ujumbe wa Wapalestina kwenye Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja na kupata kiti ndani ya ukumbi wa mikutano lakini bila kuwa na haki ya kupiga kura.