1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapalestina watano wauawa katika Ukingo wa Magharibi

23 Julai 2024

Wapalestina watano wameuwawa kwa ndege zisizo na rubani za Israel katika eneo la Tulkarm. Vyombo vya habari vya Palestina vimesema miongoni mwa waliuwawa ni wapiganaji watatu, wikiwemo makamanda wawili.

Gaza
Wapalestina watano wauawa kwa droni katika Ukingo wa MagharibiPicha: Abdel Kareem Hana/AP Photo/picture alliance

Inaelezwa kuwa maafisa waandamizi wa tawi la kijeshi la Hamas na Brigedi za al-Aqsa wa shirika la Fatah la Rais wa Palestina Mahmud Abbas wameuwawa. Jeshi la Israel lilithibitisha kwamba droni ililenga kile ilichokiita magaidi huko Tulkarm.

Hali katika Ukingo wa Magharibi imekuwa mbaya zaidi tangu kuanza kwa Vita vya Gaza kufuatia mauaji ya Hamas ya Oktoba 7 katika ardhi ya Israel.

Mwanajeshi mmoja wa Israel auawa Ukingo wa Magharibi

Kwa mujibu wa wizara ya Afya katika eneo la Ukanda wa Gaza tangu wakati huo, zaidi ya Wapalestina 550 wameuawa kutokana na operesheni za kijeshi za Israel.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW