1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapalestina watoa masharti ya kuweka chini silaha

7 Desemba 2003
KAIRO: Yale mashauriano ya makundi muhimu ya Kipalestina hayakuleta matokeo yoyote yanayoweza kukubaliwa na serikali ya Israel kama msingi wa kuanzisha mazungumzo ya mapatano. Katika mkutano wao kwenye mji mkuu wa Misri, makundi kumi na mbili yenye siasa wastani na siasa kali, yaliwafikiana kwamba kufuatana na masharti fulani yako tayari kufanya mapatano ya kusitisha mashambulio yao ya kujitolea mhanga maisha nchini Israel. Mapatano hayo hayawaingizi wanajeshi wa Israel wala walowezi wa makazi ymapatano yenyewe yatawezekana tu ikiwa Israel itaahidi kuwa haitofanya mashambulio yake tena katika ardhi za Kipalestina. Upande wake, ikituwama taarifa zake juu ya habari za maafisa wa serikali Redio Israel imearifu kwamba mashauri hayo hayatoi msingi wowote wa kuanzishwa mazungumzo mapya kuhusu mapatano ya kuwekwa chini silaha.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW