1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Wapalestina wawili wauawa kwenye operesheni ya kijeshi

2 Januari 2023

Maafisa wa afya mjini Ramallah wamesema leo kuwa wanaume wawili raia wa Palestina wameuawa katika oparesheni ya jeshi la Israel katika Ukingo wa Magharibi.

Wahlen in Israel
Picha: Nasser Ishtayeh/ZUMA/IMAGO

Wanaume hao wenye umri wa miaka 22 na 25, walipoteza maisha katika kijiji kimoja kilichoko karibu na mji wa Palestina wa Jenin. Watu wengine watatu walijeruhiwa katika oparesheni hiyo.

Kulingana na vyanzo vya jeshi, wanajeshi waliingia kwenye kijiji hicho ili kuharibu nyumba za Wapalestina wawili wanaoshukiwa kuhusika na tukio la mwezi Septemba ambapo mwanajeshi wa Israel aliuawawa.

Kituo cha redio cha jeshi la Israel kimeripoti kutokea kwa ufyatulianaji wa risasi katika mji huo wa Jenin, ambao unachukuliwa kuwa moja ya ngome za wanamgambo wa Kipalestina.

Kulingana na mamlaka katika mji wa Ramallah, jumla ya Wapalestina 172 waliuawa mwaka uliopita katika mashambulizi, idadi hiyo ikiwa kubwa tangu mwaka 2006.