1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Wapalestina zaidi ya 10 wauwawa kwa shambulio la Israel

6 Novemba 2023

Idadi ya Wapalestina waliouwawa Gaza kufuatia mashambulizi ya jeshi la Israel, imeongezeka na kufikia zaidi ya watu elfu 10.

Majeruhi wakitolewa katika gari la wagonjwa baada ya shambulio la Israel Gaza
Majeruhi wakitolewa katika gari la wagonjwa baada ya shambulio la Israel GazaPicha: Adel Al Hwajre/picture alliance/ZUMAPRESS

Idadi ya Wapalestina waliouwawa katika Ukanda wa Gaza tangu vilipoanza vita kati ya wanamgambo wa Hamas na Israel imefikia watu 10,022 kwa mujibu wa wizara ya afya katika ukanda huo.

Zaidi ya wengine 25,000 wamejeruhiwa. Maelfu ya wanawake na watoto na vijana ni miongoni mwa waliokufa kutokana na mashambulizi yanayofanywa na jeshi la Israel dhidi ya ukanda huo wa Gaza.

Vita hivyo vilichochewa na mashambulio yaliyofanywa na Hamas katika ardhi ya Israel, yaliyosababisha mauaji ya waIsrael 1,400 October 7.

Soma pia:Papa Francis akutana na viongozi wa dini ya kiyahudi

Ama kwa upande mwingine serikali ya Hamas katika ukanda huo wa Gaza imesema kivuko cha  Rafah kati ya Gaza na Misri kimefunguliwa leo kuwaruhusu raia wakigeni kuondoka Gaza pamoja na watu wenye uraia pacha na Wapalestina waliojeruhiwa.

Israel imeongeza mashambulizi yake ya ardhini dhidi ya Gaza kama sehemu ya operesheni zake za kijeshi za kujibu mashambulizi ya Hamas ya Oktoba 7.

Viongozi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wanataka mashambulio ya Israel dhidi ya Gaza yasitishwe ili kutoa nafasi kwa shughuli za misaada ya kibinadamu.
 

Mzozo wa Mashariki ya Kati wakaribia mwezi mmoja

01:17

This browser does not support the video element.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW