1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapatanishi wa Israel na Hamas wazungumza Cairo

5 Oktoba 2025

Wapatanishi wa Israel na Hamas wamekusanyika Jumapili mjini Cairo kwa mazungumzo ya kujaribu kumaliza mzozo wa takriban miaka miwili huko Gaza.

Doha | Waziri Mkuu wa Qatar Mohammed bin Abdulrahman al-Thani
Waziri Mkuu wa Qatar Mohammed bin Abdulrahman al-Thani akizungumza na waandishi wa habari mjini DohaPicha: Qatari Foreign Ministry/UPI Photo/Newscom/picture alliance

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameelezea matumaini ya mateka kuachiliwa ndani ya siku chache zijazo.

Msukumo huu mpya wa kidiplomasia unafuatia hatua ya kundi la Hamas kutangaza kukubaliana na  mpango wa amani wa rais Donald Trump wa Marekani unaojumuisha kuachiliwa huru kwa mateka wa Israel pamoja na mamia ya Wapalestina wanaoshikiliwa katika jela za Israel. Ikulu ya White House imesema kuwa Trump ametuma wajumbe wawili nchini Misri ambao ni mkwe wake Jared Kushner na mjumbe wa  Mashariki ya Kati Steve Witkoff.

Vyombo vya habari vyenye mafungamano na serikali ya Misri vimesema pande zinazozozana zitafanya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja leo na kesho Jumatatu, kabla ya tarehe ya kuadhimisha mwaka wa pili wa shambulio la Oktoba 7 la  Hamas  ambalo lilisababisha kuzuka kwa vita hivi. Licha ya miito ya Trump, Israel hata hivyo imeendeleza mashambulizi yake katika Ukanda wa Gaza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW