Waperu walalamika misaada inakawia
18 Agosti 2007Matangazo
Tetemeko kubwa la siku ya Jumatano,limeua hadi watu 510 na kama 1,500 wengine wamejeruhiwa.Vile vile maelfu ya watu wamepoteza makazi yao.Maafisa nchini Peru wana hofu kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka kwa sababu ni shida kwenda katika vijiji vingi vilivyotengwa kutokana na uharibifu wa tetemeko la ardhi la siku ya Jumatano.
Walionusurika wanalalamika kuwa misaada ya dharura inakawia kuwafikia na baadhi yao wamepora maduka ya dawa na kupigana katika foleni za kungojea chakula.Kamisheni ya Umoja wa Ulaya inatoa msaada wa dharura wa Euro milioni moja.