1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapiga kura barani Ulaya washiriki uchaguzi wa bunge

Sylvia Mwehozi
8 Juni 2024

Takriban raia milioni 400 wa Umoja wa Ulaya wanaendelea na zoezi la upigaji kura leo, kuwachagua wajumbe wa Bunge la Ulaya, katika mojawapo ya matukio makubwa ya kidemokrasia duniani.

Uchaguzi wa bunge la Ulaya 2024
Uchaguzi wa bunge la Ulaya Jamhuri ya CzechPicha: Ondrej Deml/CTK Photo/picture alliance

Takriban raia milioni 400 wa Umoja wa Ulaya wanaendelea na zoezi la upigaji kura leo, kuwachagua wajumbe wa Bunge la Ulaya, katika mojawapo ya matukio makubwa ya kidemokrasia duniani.

Vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia vinatafuta kupata uungwaji mkono zaidi katikati mwa ongezeko la gharama za maisha na kutoridhika kwa wakulima. Vita vya Gaza na Ukraine pia ni miongoni mwa masuala yanayojadiliwa mno.

Uchaguzi wa Bunge la Ulaya hufanyika kila baada ya miaka mitano katika jumuiya hiyo yenye wanachama 27.

Uchaguzi huo ulianza Alhamisi wiki hii nchini Uholanzi na utakamilika siku ya Jumapili, wakati nchi nyingi zitakapokamilisha zoezi la uchaguzi. Matokeo ya awali yataanza kutolewa jioni baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa katika nchi zote wanachama.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW