1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapiga kura wa Uholanzi wanateremka vituoni leo kuipigia kura katiba ya umoja wa ulaya

1 Juni 2005

The Hague

Waziri mkuu wa Uholanzi,Jan Peter BALKENENDE amewatolea mwito kwa mara nyengine tena wapiga kura waunge mkono katiba ya umoja wa ulaya,.masaa machache kabla ya vituo vya uipigaji kura kufunguliwa hii leo nchini humo.“Mustakbal wa Uholanzi unakutikana barani Ulaya“ ameshadidia waziri mkuu huyo.Wapiga kura milioni 13 wanatakiwa waipigie kura katiba ya umoja wa ulaya.Utafiti wa maoni ya umma uliofanywa hivi karibuni umeonyesha idadi ya wanaoipinga katiba hioyo iko juu sawa na ilivyooshuhudiwa nchini Ufaransa.Ingawa matokeo ya kura hiyo ya maoni si lazma yaheshimiwe,hata hivyo vyama vya kisiasa nchini Uholanzi vimeahidi kutilia maanani matokeo hayo ikiwa idadi ya wapiga kura itapindukia asili mia 30.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW