Wapiga kura wachagua bunge jipya Afghanistan
18 Septemba 2010Matangazo
Hata hivyo, Wizara ya Mambo ya Ndani katika mji mkuu Kabul imesema kuwa imeridhika na zoezi hilo la uchaguzi.
Muda mfupi tu baada ya kufunguliwa kwa vituo vya kupigia kura, Rais Hamid Karzai mara nyingine tena alitoa mwito kwa Waafghanistan kujitokeza kupiga kura zao.
Wagombea 2,500 wamewania viti 248 bungeni katika uchaguzi mkuu wa pili kufanywa nchini humo tangu serikali ya Taliban kupinduliwa mwaka 2001. Uchaguzi huo umefanywa chini ya ulinzi mkali.
Kiasi ya watu milioni 10.5 wamekuwa na haki ya kupiga kura katika uchaguzi huo unaotazamwa kama ni mtihani mkuu wa utulivu na mchakato wa kidemokrasia nchini Afghanistan.Matokeo ya uchaguzi hayatazamiwi kabla ya mwisho wa mwezi wa Oktoba.
Mwandishi: P.Martin/ ZPR
Mpitiaji: M.Dahman