Wapiganaji 50,000 wa Tigray waachishwa shughuli za kijeshi
27 Julai 2023Matangazo
Kulingana na televisheni ya eneo hilo Tigray TV, taarifa hiyo imetolewa na naibu mkuu wa serikali ya mpito ya jimbo hilo Jenrali Tadesse Worede, aliyekuwa mkuu wa jeshi la Tigray wakati wa mapigano hayo.
Vyombo vya habari vilivyo karibu na pande zote mbili vilitangaza kwamba hatua hiyo ya kuwaondoa wapiganaji katika shughuli za upiganaji ilianza mnamo Mei 26.
Soma zaidi: Marekani yasimamisha misaada ya chakula nchini Ethiopia
Kwa sasa mapigano yamesitishwa na majeshi ya Eritrea yaliyokuwa yameingia Tigray kuliunga mkono jeshi la Ethiopia, yameondoka kutoka kwenye jimbo hilo.