1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapiganaji 8 wameuwawa kwa mashambulizi ya anga ya Urusi

21 Agosti 2023

Takriban wapiganaji wanane wameuwawa na mashambulizi ya Urusi katika ngome ya mwisho ya waasi kaskazini Magharibi mwa Syria.

Shirika linalofuatilia hali ya haki za binadamu nchini Syria lenye makao yake Uingereza limesema madege ya kivita ya Urusi yameshambulia makao makuu ya kundi la Hayat Tahrir al Sham ambalo linadhibiti eneo kubwa la mkoa wa Idlib nchini Syria.Mashambulizi hayo yamefanyika alfajiri ya leo Jumatatu na yamesababisha watu wengi kujeruhiwa.Imeelezwa kwamba madege ya kivita ya Urusi  yamekuwa yakizidisha mashambulizi dhidi ya maeneo ya waasi katika eneo hilo la Idlib na maeneo mengine ya vijijini.Urusi na Iran zinamuunga mkono Rais Bashar al Assad wa Syria wakati Uturuki imekuwa ikiviunga mkono baadhi ya vikosi vya wapinzani tangu lilipoanza vuguvugu dhidi ya utawala wa Assad mwaka 2011.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW