1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Ugaidi

Wapiganaji 9 na kamanda wauwawa kwa mashambulizi Syria

26 Machi 2024

Shirika moja la kutetea haki za binadamu limesema yapata wapiganaji tisa wa wanaoiunga mkono Iran akiwemo kamanda, wameuwawa katika mashambulizi ya angani mashariki mwa Syria Jumanne

Shambulizi la Syria limeuwa wapiganaji tisa upande wa mashariki
Shambulizi la Syria limeuwa wapiganaji tisa upande wa masharikiPicha: Omar Albam/DW

Shirika la Syrian Observatory for Human Rights linasema, mashambulizi hayo yalikuwa yanailenga nyumba waliyokuwa wanaishi ambaoy pia ilikuwa kama kituo cha mawasiliano na zaidi ya watu 20 wamejeruhiwa.

Shirika hilo lililo na makao yake Uingereza linasema halifahamu aliyefanya mashambulizi hayo na hakuna kundi lililojitokeza kudai kuhusika.

Soma pia; UN: Wasyria wanaorejea nyumbani wanakabiliwa na unyanyasaji

Israel imefanya mamia ya mashambulizi yanayoyalenga makundi yanayoiunga mkono Iran ambayo yanapigana kwa pamoja na majeshi ya Rais Bashar al-Assad, katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo vilivyodumu kwa zaidi ya mwongo mmoja.

Vyombo vya habari vilivyo karibu na serikali ya Syria vinasema mashambulizi hayo yamefanywa na Marekani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW