1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapiganaji wa Wagner hawajaondoka Jamhuri ya Afrika ya Kati

9 Julai 2023

Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Afrika ya kati amesema leo kuwa kuondoka kwa mamia ya wapiganaji wa kundi la Wagner ni sehemu ya utaratibu wa kufanya kazi kwa mzunguko na, si kuwa wameondolewa nchini humo.

 Zentralafrikanische Republik Denkmal zu Ehre der "Wagner-Gruppe" in Bangui
Picha: Barbara Debout/AFP

Msemaji huyo wa serikali Albert Yaloke Mokpem ameongeza kuwa, baadhi ya wapiganaji hao wameondoka na wengine wanatarajiwa kwenda nchini humo.

Uasi wa kiongozi wa kundi hilo Yevgeny Prigozhin nchini Urusi, umezua maswali kuhusu mustakabali wa Wagner na operesheni zake Afrika ya kati, Mashariki ya kati, na maeneo mengine ya bara la Afrika. Wapiganaji wa kampuni hiyo wamekuwa wakishirikiana na serikali ya Jamhuri ya Afrika ya kati kukabiliana na makundi ya waasi tangu mwaka 2018.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW