Wapiganiaji uhuru Kenya wamtaka Mfalme Charles kuomba radhi
31 Oktoba 2023Mfalme Charles anakabiliwa na miito ya kumtaka aombe radhi kuhusiana na historia ya umwagaji damu uliosababishwa na ukoloni wa nchi yake, Uingereza.
Hii ni ziara ya kwanza ya kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 74 katika taifa la Kiafrika na Jumuiya ya Madola tangu alipovishwa taji la ufalme mwezi Septemba 2022 baada ya kifo cha mama yake, Malkia Elizabeth II.
Soma zaidi: Mfalme Charles III ziarani Kenya
Ulimwengu wamuaga Malkia Elizabeth II
Mfalme Charles na mkewe, Camilla, walikaribishwa katika hafla rasmi asubuhi ya Jumanne (Oktoba 31) na Rais wa Kenya William Ruto katika Ikulu ya Nairobi.
Ruto aliisifu ziara hiyo akisema ni fursa muhimu ya kuimarisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali.
Hata hivyo, alisema anatambua mambo machungu zaidi ya uhusiano wa kihistoria kati ya Uingereza na Kenya.
Nchi hiyo ya Afrika Mashariki inajiandaa kuadhimisha miaka 60 ya uhuru kutoka kwa Uingereza Desemba mwaka huu.