Wapinzani wapanga maandamano makubwa Senegal
9 Februari 2024Dazeni kadhaa za makundi ya kidini na kiraia na mashirika ya kitaaluma, ambayo yameungana katika vuguvugu jipya, yametoa wito kwa watu kuhudhuria swala ya Ijumaa wakiwa wamevalia mavazi meupe na rangi za taifa.
Wakaazi wa mji mkuu wa Dakar, pia wamehimizwa kupitia mitandao ya kijamii, kuandamana baadae leo, kwenye uwanja mkubwa ulioko karibu na mji mkuu.
Soma zaidi: Wabunge wakamatwa wakipinga kuahirishwa uchaguzi Senegal
Utambulisho wa walioitisha maandamano hayo haujabainishwa, lakini wagombea wengi wa uchaguzi ulioahirishwa wametanga kuwa wanapanga kujiunga na maandamano hayo.
Bunge la Senegal liliunga mkono uamuzi wa ghafla wa Sall kusogeza uchaguzi uliokuwa ufanyike tarehe 25 mwezi huu, na kusababisha hasira za wapinzani na wasiwasi wa kimataifa.