1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waranti mpya wa ICC nchini Libya waandaliwa

Sekione Kitojo
6 Mei 2020

Mwendesha mashitaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu alisema Jumanne kwamba ofisi yake inafanyakazi kutayarisha waranti mpya nchini Libya, akizungumzia idadi ya juu ya vifo vya raia kutokana na mashambulizi.

Niederlande Chefanklägerin beim Internationalen Strafgerichtshof in Den Haag | Fatou Bensouda
Picha: Getty Images/AFP/E. Plevier

Wakati huo huo mwendesha mashtaka huyo alisisitiza kwamba makamanda wa jeshi huenda watawajibishwa kwa uhalifu uliofanywa na majeshi yao.

Fatou Bensouda aliliambia baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba Libya inabaki kuwa muhimu kwa ofisi yake. Amedokeza kwamba mashambulizi yaliyoanzishwa mwaka mmoja uliopita na majeshi yaliyoko upande wa mashariki chini ya kamanda wa jeshi Khalifa Haftar kujaribu kuukamata mji mkuu Tripoli, yanaendelea.

Amesema ofisi yake inaangalia matukio, hususan vifo vya raia kutokana na mashambulizi ya anga na makombora na matukio ambayo huenda yanaweza kufikia kuwa uhalifu chini ya sheria za mkataba wa Roma ambao uliunda mahakama ya kimataifa ya uhalifu.

Libya imeshuhudia vurugu tangu mwaka 2011

Bensouda hakumtaja mtu yeyote kuwa ana uweza kukamatwa kwa kutumia waranti hizo. Lakini alisema kwa kuwalenga raia kwa makusudi, „ni uhalifu wa kivita chini ya sheria za mkataba wa Roma,"

Libya imekuwa katika vurugu tangu mwaka 2011, wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipouangusha utawala wa Moamar Gadafi, ambaye baadaye aliuwawa. Nchi hiyo tangu wakati huo imegawanyika kati ya tawala hasimu upande wa mashariki na magharibi, kila upande ukiungwa mkono na makundi yenye silaha.

Mwanajeshi wa Lebanon akiwa mbele ya gari linateketea mjini TripoliPicha: Getty Images/AFP/I. Chalhoub

Mashambulizi ya Haftar pia yanaungwa mkono na Ufaransa, Urusi, Jordan, Umoja wa Falme za Kiarabu pamoja na mataifa mengine muhimu ya Kiarabu, serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa mjini Tripoli inaungwa mkono na Uturuki, Italia na Qatar.

Balozi ya Umoja wa Mataifa nchini Libya Taher El-Sonni amemshutumu Haftar kwa kufanya uhalifu wa kivita, ambao Bensouda amedokeza na kuliambia baraza la Usalama mwendesha mashitaka wa jeshi la serikali ametoa waranti wa kukamatwa Haftar pamoja na viongozi wengine chini ya uongozi wake.

Nchi inastahili kuwajibika pamoja na maafisa nje ya Libya

„Ni kitu gani ICC inasubiri kuwawajibisha wale wote wanaohusika na ukiukaji huu ambao umeelezwa hii leo ambao umefanywa na kile kinachoitwa Jeshi la taifa, linaloongozwa na Haftar? Ameuliza.

Aidha alisema ni lazima pia kwa nchi kuwajibika pamoja na maafisa nje ya Libya ambao wanaunga mkono na kugharamia ukiukaji huo pamoja na mamluki kutoka mataifa kadhaa ambao wanafanya ukiukaji huo.

Bensouda (kulia) akiwa majukumuni mahakama ya ICCPicha: Reuters/P. van de Wouw

Akizungumza kwa njia ya vidio, Bensouda alisema ofisi yake pia inafuatilia uchunguzi kuhusiana na „matatizo makubwa na yanayoendelea „ ya watu kuwekwa kizuwizini kiholela pamoja na matendo mabaya wanayotendewa wahamiaji na wakimbizi wanaojaribu kupitia nchini Libya. Amesema taarifa zinaonesha kuwa watu ambao wamewekwa kizuwizini bila ulinzi sahihi wameteswa na kuuwawa na kwamba wanaume, wanawake na watoto wamebakwa pamoja na njia nyingine za matumizi ya nguvu ya ngono.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW