1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Warohingya wakumbuka miaka sita ya mauaji ya halaiki

25 Agosti 2023

Maelfu ya Waislamu wa jamii ya Rohingya wameandamana katika kambi za wakimbizi kusini mwa Bangladesh katika maadhimisho ya sita ya mauaji ya halaiki dhidi yao.

Cox's Bazar, Rohingya, Bangladesh
Picha: DW

Wakimbizi hao wanataka haki itendeke kufuatia kamatakamata na mauaji yaliyofanywa na jeshi la Myanmar dhidi yao miaka sita iliyopita.

Kiongozi wao, Mohammad Jubair, aliliambia kundi la wakimbizi katika kambi ya Kutupalong kwamba jamii ya kimataifa haijawatendea haki.

Soma zaidi: Watu 6 wauwawa katika makabiliano kwenye kambi ya wakimbizi Bangladesh
Warohingya Bangladesh huenda wakakabiliwa na utapiamlo

Shirika la amani na haki za binaadamu la Arakan Rohingya ndilo lililoandaa maandamano hayo katika kambi 34 za wakimbizi, ambazo ni makao ya zaidi ya Warohingya milioni moja waliokimbia mateso nchini kwao, Myanmar. 

Myanmar haiwatambui sehemu kubwa ya jamii hiyo ya Waislamu, linalotajwa kuwa kundi kubwa la watu duniani lisilotambuliwa uraia wao na taifa lolote.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW