WARSAW: Jengo la ukumbusho wa maisha ya Wayahudi
27 Juni 2007Matangazo
Poland itajenga jumba jipya la makumbusho kwa heshima ya maisha ya Wayahudi nchini humo,kabla ya kuteketezwa katika maangamizi makuu wakati wa Vita vya Pili vya Dunia.Rais Lech Kaczynski wa Poland na viongozi wa Kiyahudi,waliweka msingi wa Jumba la Ukumbusho la Historia ya Wayahudi wa Poland,mjini Warsaw.Jumba hilo la ukumbusho litafunguliwa katika kipindi cha miaka miwili ijayo.Kabla ya vita,zaidi ya Wayahudi milioni tatu walikuwa wakiishi katika mji mkuu wa Poland, Warsaw uliokuwa kiini cha jumuiya ya Wayahudi wa Ulaya.