WARSAW : Maaskofu na makasisi kuchunguzwa
13 Januari 2007Matangazo
Kanisa Katoliki nchini Poland limesema litawachunguza maskofu wake wote na makasisi ili kujuwa iwapo wameshirikiana na mashuhu wakati wa enzi ya ukomunisiti nchini humo.
Uamuzi huo umepitishwa kwenye mkutano wa maaskofu uliotishwa kufuatia kujiuzulu kwa askofu mkuu wa Warsaw hapo Jumapili.Askofu Mkuu Stanislaw Wielgus amejiuzulu baada ya kukiri kuwafanyia upelelezi makachero wakati wa utawala wa kikomunisti.Mchungaji wa kanisa kuu la Krakow Janusz Bielanski alijiuzulu siku moja baadae kwa sababu hiyo hiyo.
Kuungama huko kumesababisha kashfa nchini Poland ambapo Kanisa Katoliki lilikuwa likiheshimiwa sana kam