WARSAW: Mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto yaanza nchini Poland
24 Oktoba 2005Matangazo
Chama cha sheria na haki nchini Poland kimeanzisha mazungumzo ya kuunda serikali mpya ya mseto, siku moja baada ya mgombea wake, Lech Kachinski, kuchaguliwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo. Mbunge mashuhuri nchini Russia amesema kuchaguliwa kwa Kachinski kuwa rais wa Poland huenda kukafungua njia ya uhusiano mwema kati ya Poland na Russia, lakini huenda kukasababisha tatizo kubwa barani Ulaya.