WARSAW: Poland kuondoa majeshi kutoka Irak?
18 Novemba 2007Matangazo
Waziri Mkuu mpya wa Poland bwana Donald Tusk ametangaza kuwa nchi yake itaondoa majeshi kutoka Irak mwaka ujao.
Akizungumza katika mahojiano ya radio waziri wake wa ulinzi amesema kuwa wanajeshi 900 wa nchi yake ambao sasa wapo Irak watarudishwa nyumbani mwakani.
Habari zaidi juu ya uamuzi huo zitatolewa ijumaa ijayo na waziri mkuu bwana Tusk atakapofafanua sera za serikali yake mpya bungeni.
Poland ni miongoni mwa nchi zilizofungamana thabiti na Marekani, na uhusiano baina ya nchi mbili hizo uliimarika katika kipindi cha miaka miwli iliyopita kabla ya uchaguzi wa hivi karibuni ambapo chama cha waziri mkuu Donald Tusk kilishinda kutokana na kuahidi kuyaondoa haraka majeshi ya Poland kutoka Irak.