1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WARSAW Rais wa Ujerumani afanya ziara nchini Poland

30 Agosti 2005

Rais wa Ujerumani bwana Horst Köhler leo anaanza ziara ya siku tatu nchini Poland.

Rais Köhler anatarajiwa kulakiwa na mwenyeji wake rais Aleksander Kwasniewsk na baadaye kwa pamoja wataweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya ubalozi wa Ujerumani mjini Warsaw.

Bwana Köhler pia ataweka mashada ya maua kwenye kaburi la askari asiyejulikana , kwenye kumbukumbu ya kitongoji cha wayahudi na katika kumbukumbu ya upinzani dhidi ya mafashisti.

Rais wa Ujerumani pia atashiriki katika maadhimisho ya miaka 25 ya jumuiya ya wafanyakazi”,Solidarity” iliyouangusha utawala wa kikomunisti nchini Poland na kuweka msingi wa mabadiliko makubwa ya kisiasa barani Ulaya, ikiwa pamoja na kuangushwa kwa kuta la Berlin.

.