WARSAW. Rais wa Ujerumani ziarani Poland
31 Agosti 2005Matangazo
Rais Horst Köhler wa Ujerumani leo yumo katika siku yake ya pili ya ziara nchini Poland ambako anatarajiwa kuhudhuria sherehe zakuadhimisha miaka 25 tangu kuundwa kwa jumuiya ya wafanyikazi inayoitwa Solidarity.
Mwenyeji wake rais Aleksander Kwasniewski alifanya mazungumzo na rais Köhler na viongozi wote wawili wamesisitiza umuhimu wa kuzungumza kwa uwazi juu ya matatizo ya awali baina ya nchi hizi mbili.
Vile vile rais Köhler aliweka shada la mauwa kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya vita ya pili ya dunia kwenye kitongoji cha wayahudi.
Baadae rais wa Ujerumani Horst Köhler anatarajiwa kuhudhuria maadhimisho ya miaka 66 tangu Ujerumani ilipo ivamia Poland.