WARSAW : Uchaguzi wa mapema Poland
10 Agosti 2007Matangazo
Rais wa Lech Kaczynski wa Poland na kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Donald Tusk wamesema kwamba uchaguzi wa mapema nchini humo limekuwa jambo lisiloweza kuepukwa.
Msemaji wa rais amewaambia waandishi wa habari kwamba wameona uchaguzi huo yumkini ukafanyika katika kipindi kinachokuja cha majira pukutizi.Msemaji huyo alikuwa akizungumza baada ya rais kuwa na mazungumzo ya faragha ya masaa manne na kiongozi wa upinzani.
Poland ilitumbukia kwenye mashaka ya kisiasa mwezi uliopita wakati Waziri Mkuu Jaroslaw Kaczysnki alipomtimuwa kiongozi wa chama kidogo kutoka serikali ya mseto.