WARSAW.wachimba mgodi wa Poland bado hawajaokolewa
22 Novemba 2006Matangazo
Hali ya wachimba mgodi 15 walionaswa chini ya mgodi nchini Poland baada ya mlipuko hapo jana bado haijajulikana mpaka sasa.
Juhudi za kuwafikia wachimba mgodi hao walio kilomita moja chini ya ardhi zinatatizwa na kiwango cha juu cha gesi ya Methane iliyo tapakaa.
Watu wanane waliuwawa pia katika mlipuko huo wa gesi dhidi ya mgodi wa mji wa Katowice kusini mwa Poland.
Waokowaji wanasema kuwa huenda mlipuko mwingine wa gesi ukatokea na hali hiyo inasababisha wasiwasi katika kuendelea na juhudi za kuwaokowa wachimba mgodi waliokwama ardhini.