1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaItaly

Wasafiri waokolewa kutoka treni iliyoshika moto Austria

8 Juni 2023

Wasafiri zaidi ya 151 wameokolewa kutoka katika treni iliyoshika moto ikipita katika njia ya chini ya milima kwenye jimbo la Tyrol nchini Austria

Brand in Tiroler Bahntunnel
Picha: ZOOM.TIROL/APA/AFP

Treni hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka Innsbruck nchini Austria, kuelekea Hamburg Ujerumani kupitia Amsterdam, Uholanzi. Mamlaka katika eneo la tukio zimesema idadi iliyotangazwa awali ilikuwa ya juu zaidi kwa sababu ilitokana na data za waliokata tiketi, na kwamba ilirekebishwa baada ya polisi kuwahesabu wasafiri walioondolewa ndani ya treni iliyokumbwa na mkasa. Wafanyakazi wa huduma za dharura wamesema wasafiri 33 walipatiwa matibabu kutokana na majeraha madogo waliyoyapata.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW