1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMarekani

Wasayansi wa Marekani watunukiwa tuzo ya Nobel ya Kemia

4 Oktoba 2023

Wanasayansi watatu wa Marekani wametunukiwa Tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka huu kwa ugunduzi wao wa chembe ndogo za atomi zilizoleta mapinduzi katika teknolojia mamboleo inayofahamika kama LED.

Wanasayansi watatu wa Marekani Moungi Bawendi, Louis Brus na Alexei Ekimov watunukiwa Tuzo ya Nobel ya Kemia
Wanasayansi watatu wa Marekani Moungi Bawendi, Louis Brus na Alexei Ekimov watunukiwa Tuzo ya Nobel ya KemiaPicha: Jonathan Nackstrand/AFP

Teknolojia hiyo inatumika kwenye uundaji wa runinga na taa za kisasa pamoja na vifaa vya kitaalamu vinavyotumika kwenye upasuaji.

Wasayansi hao Moungi Bawendi, Louis Brus na Alexei Ekimov kutoka vyuo vikuu vitatu nchini Marekani wametangazwa washindi hii leo wa tuzo hiyo mashuhuri yenye thamani ya dola milioni 1.

Mjumbe wa kamati ya tuzo za Nobel Pernilla Witting amesema mchango wa wasayansi hao umewezesha kutumika chembe ndogo za atomi ambazo hazionekani kwa macho lakini zinatoa mwanga pamoja na rangi.

Wote watatu wamesema wamepokea kwa bashasha na mshangao tangazo la kuteuliwa kwao kuwa washindi wa tuzo hiyo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW