1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washauri wa rais Obama wakutana kuijadili Syria

24 Agosti 2013

Washauri wa rais Barack Obama watakutana katika ikulu ya Marekani ya White House mwishoni mwa wiki hii kujadili nafasi mbali mbali za nchi hiyo, ikiwa ni pamoja na hatua za kijeshi, dhidi ya serikali ya Syria.

People, affected by what activists say is nerve gas, are treated at a hospital in the Duma neighbourhood of Damascus August 21, 2013. Syrian activists accused President Bashar al-Assad's forces of launching a nerve gas attack on rebel-held districts near Damascus on Wednesday that they said killed more than 200 people. There was no immediate comment from Syrian authorities, who have denied using chemical weapons during the country's two-year conflict, and have accused rebels of using them, which the rebels deny. REUTERS/Bassam Khabieh (SYRIA - Tags: POLITICS CIVIL UNREST CONFLICT)
Wahanga wa gesi ya sumu nchini Syria wakipatiwa matibabuPicha: Reuters

Washauri wa rais Barack Obama watakutana katika ikulu ya Marekani ya White House mwishoni mwa wiki hii kujadili nafasi mbali mbali za nchi hiyo , ikiwa ni pamoja na hatua za kijeshi , dhidi ya serikali ya Syria.

Mjadala huo utahusu iwapo serikali ya Syria ilitumia silaha za kemikali katika shambulio mapema wiki hii.

Rais Barack ObamaPicha: Reuters

Maafisa wa Marekani wamesema jana Ijumaa(23.08.2013) kwamba iwapo rais Obama atashiriki katika mkutano huo , hali inayoonekana kuwa kuna uwezekano , itakuwa kikao chake cha kwanza kamili akiwa na wasaidizi wake wa ngazi ya juu wa sera za mambo ya kigeni tangu shambulio la gesi ya sumu siku ya Jumatano katika kitongoji kimoja mjini Damascus.

Uamuzi bado

Lakini afisa huyo ambaye amezungumza kwa masharti ya kutotajwa jina, ametahadharisha dhidi ya matarajio kuwa uamuzi wowote wa mwisho huenda unaweza kutolewa katika duru hii ijayo ya majadiliano.

Wakati huo huo wizara ya ulinzi inayaweka tayari majeshi yake iwapo rais Barack Obama ataamua kuchukua hatua ya kijeshi dhidi ya Syria, amesema waziri wa ulinzi wa Marekani Chuck Hagel siku ya Ijumaa.

Waziri wa ulinzi wa Marekani Chuck HagelPicha: Getty Images

Huku kukiwa na miito kadha ya kujingilia kati kijeshi baada ya utawala wa Syria kutumia kile kinachodaiwa kuwa ni silaha za kemikali wiki hii, makamanda wa jeshi la Marekani wamenajitayarisha kwa uwezekano mbali mbali kwa rais Obama iwapo ataamua kuanzisha mashambulio dhidi ya utawala wa Syria, Hagel amewaambia waandishi habari akiwa katika ndege yake iliyokuwa ikielekea nchini Malaysia.

Lakini amekataa kutoa taarifa zaidi kuhusiana na wapi majeshi ya Marekani yatawekwa pamoja na vifaa huku kukiwa na hali ya kuongezeka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.

"Wizara ya ulinzi inawajibu wa kumpa rais uwezekano kwa kila aina ya hali," Amesema Hagel.

Manowari ya jeshi la MarekaniPicha: picture alliance / dpa

Meli zawekwa katika tahadhari

Amesema wakati afisa wa wizara ya ulinzi akisema kuwa jeshi la majini litapanua uwapo wake katika bahari ya Mediterranean kwa kuweka meli ya nne ikiwa na uwezo wa kubeba makombora.

Kikosi cha sita cha jeshi la Marekani , kikiwa na wajibika katika bahari ya Mediterranean , kimeamua kuibakisha manowari ya USS Mahan katika eneo hilo badala ya kuiruhusu kurejea nyumbani katika bandari ya Norfolk , jimboni Virginia.

Manowari nyingine tatu hivi sasa zimewekwa katika eneo hilo, USS Gravely , USS Barry na USS Ramage. Meli zote nne za kivita zina makombora kadha ya Tomahawk.

Meli hizo za ziada zinairuhusu wizara ya ulinzi kuchukua hatua za haraka iwapo Obama ataamuru shambulio la kijeshi.

"Rais ameitaka wizara ya ulinzi kutoa mapendekezo mbali mbali. Pamoja na hayo , wizara ya ulinzi iko tayari na imekuwa tayari kutoa uwezekano wa aina yoyote kwa rais wa Marekani ," Hagel amesema.

Ndege ya kivita ya jeshi la marekani F-35Picha: picture-alliance/ap

Mkuu hiyo wa wizara ya ulinzi pamoja na maafisa wengine wa wizara ya ulinzi katika utawala wa rais Obama wameweka wazi kuwa hakuna uamuzi ulikwisha chukuliwa iwapo kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya utawala wa rais Bashar al-Assad.

Magazeti ya Marekani yamekuwa yakieleza kuwa kuna hali ya kutokubaliana ndani ya utawala wa Marekani kuhusiana na hatari ya kujiingiza katika vita vingine katika mashariki ya kati.

Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe / rtre

Mhariri : Sudi Mnette

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW