WASHINGTON: Ajali ya ndege imeua watu 49
27 Agosti 2006Matangazo
Ndege ya shirika la Comair,ikiwa na watu 50 imeanguka Kentucky nchini Marekani.Ripoti zinasema watu wote isipokuwa mmoja wamefariki. Hali ya abiria huyo ni mahututi.Kwa hivi sasa bado haijulikani nini kilichosababisha ndege hiyo kuanguka muda mfupi tu baada ya kuondoka uwanja wa ndege wa Lexington.Maafisa wa usafiri wa ndege wamesema,ndege hiyo ilikuwa ikielekea Atlanta nchini Marekani.
