1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Bush aomba fedha kupambana na mafua ya ndege.

2 Novemba 2005

Rais wa Marekani George W. Bush amelitaka baraza la Congress kuidhinisha dola bilioni 7 za dharura kuilinda nchi hiyo dhidi ya uwezekano wa kuzuka kwa maafa ya ugonjwa wa mafua ya ndege.

Akizungumza katika taasisi ya taifa ya afya , Bush amesema kuwa Marekani inatakiwa kuwa tayari katika viwango vyote iwapo kutatokea ugonjwa huo wa mafua ya ndege.

Pia amesema ni muhimu kuzalisha chanjo mpya dhidi ya maradhi hayo hatari. Ombi la Bush linakuja siku moja baada ya bata mwitu kadha kugundulika na virusi vya homa ya mafua ya ndege nchini Canada.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW