1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON :Bush atoa fedha zaidi kwa majeshi.

12 Mei 2005

Rais George Bush ameidhinisha matumizi ya dola bilioni 82 kwa ajili ya kugharimia vita nchini Irak na Afghanistan.

Sehemu kubwa ya fedha hizo itatumika kwa ajili ya kununulia zana za kivita na malipo kwa familia za askari waliokufa nchini Irak na Afghanistan.

Kiasi kingine cha fedha hizo,dola milioni mia tisa na saba kitatumika katika kuwasaidia wahanga wa maafa ya mafuriko yaliyotokea katika za bara la Asia mnamo mwezi wa desemba mwaka jana.

Wizara ya ulinzi ya Marekani ilitahadharisha hapo awali kwamba bila ya fedha hizo kuidhinishwa baadhi ya shughuli za kijeshi zisingeweza kugharimiwa hadi kufikia kati kati ya mwezi huu.

.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW