Washington: Bush na Bremer wajadili utawala
13 Novemba 2003Matangazo
Marekani imeimarisha shinikizo mbele ya Halmashauri Tawala iliyoteuliwa na Marekani nchini Iraq, kutayarisha muswada wa katiba na kuingia safari hadi kufikia kituo cha kujitawala. Mashambulizi ya kila siku na hujuma za jeshi la Marekani dhidi ya waasi, jana yalizusha mikutano ya dharura ya Rais George W. Bush pamoja na wasaidizi wake wa ngazi ya juu kuhusu sera ya mambo ya nje, ili kujadili njia za kukabidhi madaraka ya kisiasa mikononi mwa Wairak. Mkaguzi wa kiraia wa Marekani kwa Iraq, Paul Bremer, akitoka mkutanoni pamoja na Bush alisema atatuma risala ya rais ambaye, anataraji kuona matokeo ya Halmasharui ya Kiutawala nchini Iraq.
