WASHINGTON: Clinton na msaada kwa wagonjwa wa UKIMWI
9 Mei 2007Matangazo
Rais wa zamani wa Marekani,Bill Clinton amezindua makubaliano mapya pamoja na makampuni makuu ya dawa.Azma ya makubaliano hayo ni kupunguza kwa asilimia 25 hadi asilimia 50,bei ya dawa za kuwasaidia wagonjwa wa UKIMWI na walioambukizwa virusi vya HIV katika nchi zinazoendelea.Dawa hizo zitatumiwa kwa wagonjwa ambao miili yao sasa haikubaliani tena na mchanganyiko wa dawa za hapo awali.Katika taarifa iliyotolewa,Clinton amesema, kiasi ya watu milioni saba katika mabara ya Afrika,Asia na Latin Amerika wanahitaji tiba.