1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON Condoleezza Rice kulitembelea eneo la Darfur

16 Julai 2005

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Bi Condoleezza Rice atalitembelea eneo la Darfur nchini Sudan wiki ijayo. Rais George W Bush ameamuru fedha zitolewe kuwasaidia wanajeshi wa umoja wa Afrika wanaolinda amani katika eneo la Darfur.

Msemaji wa Bi Rice,Sean McCormack, ametangaza kwamba Rice ataondoka mjini Washington siku ya Jumanne kwenda Sudan akiwa njiani kuelekea Senegal kuhudhuria mkutano kuhusu uchumi. Baadaye ataondoka Senegal kwenda mashariki ya kati kufuatia machafuko yanaoendelea kuongezeka katika eneo hilo.

Hapo awali Condoleezza Rice alimtaka waziri wa ulinzi wa Israel kufanya kila awezalo kuulinda mpango wa kuyaondoa makazi ya walowezi wa kiyahudi kutoka mkanda wa Gaza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW