Washington. Kimbunga Rita kimepungua kasi.
24 Septemba 2005Kimbunga Rita kimewasili nchini Marekani katika eneo la kusini mwa pwani ya ghuba , na kushambulia jimbo la Texas na Louisiana kwa mvua kubwa.
Kimbunga Rita kimepungua nguvu yake na kuwa katika kiwango cha pili cha hatari, lakini bado kinaendelea kuvumisha upepo wenye kasi ya kilometa 200 kwa saa. Kimbunga hicho kimesababisha miji mingi kukosa umeme katika majimbo yote mawili na moto mkubwa umeripotiwa katika mji wa jimbo la Texas wa Galveston.
Eneo hilo lililoathirika na kimbunga hicho linasemekana kuwa limehamwa na wakaazi wake, baada ya zaidi ya watu milioni mbili kukimbia eneo hilo.
Wafanyabiashara ya mafuta duniani wanasubiri kuona iwapo vinu vikuu vya kusafishia mafuta vitaharibiwa na kimbunga hicho Rita.
Kimbunga Katrina na Rita vimeharibu karibu uzalishaji wote wa nishati katika ghuba ya Mexico.