1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Kimbunga Rita kimewasili Marekani.

24 Septemba 2005

Kimbunga Rita kimewasili nchini Marekani , na kushambulia jimbo la Texas na Louisiana kwa mvua kubwa na kutishia kuleta mafuriko katika maeneo ya mabondeni.

Kimbunga Rita tayari kimekwisha sababisha mafuriko mengine katika mji wa New Orleans ikiwa ni chini ya mwezi mmoja tangu pale mji huo ulipoharibiwa na kimbunga Katrina.

Upepo mkali na mawimbi makubwa yameharibu matuta ya kuzuwia maji katika wilaya kadha za mji huo.

Kimbunga Rita kimepunguzwa uwezo wake na kuwa katika kiwango cha tatu, lakini bado kinaendelea kuwa na upepo unaofikia mwendo wa kilometa 200 kwa saa.

Kaimu mkuu wa taasisi ya kushughulikia masuala ya dharura David Paulison , amesema kuwa kazi ya kuwaondoa watu zaidi ya milioni moja wakaazi wa eneo hilo inaendelea vizuri.

Hapo kabla , basi ambalo lilikuwa limewachukua wazee wanaokimbia kutoka katika eneo la kimbunga lilishika moto karibu na mji wa Dallas, Texas na kuuwa watu 24.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW