1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Madai ya kufanyiwa vitendo vya dharau kitabu kitakatifu kwa Waislamu cha Koraan yapata nguvu baada ya jeshi la Marekani kukiri kuwapo vitendo hivyo

28 Mei 2005

.

Maelfu ya watu katika maeneo yenye Waislamu duniani wamefanya maandamano dhidi ya madai ya kufanyiwa vitendo kinyume na utaratibu kitabu kitukufu wa Waislamu Koraan, kitendo kilichofanywa na wanajeshi wa Marekani katika kituo cha kijeshi cha kuwaweka mahabusu huko Guantanamo Bay.

Waandamanaji nchini Misr, Pakistan , Jordan, Lebanon na Malaysia wanadai serikali ya Marekani iombe radhi na kuwaadhibu wale waliohusika.

Maandamano hayo yamekuja baada ya jeshi la Marekani kukiri kuwa baadhi ya walinzi wake wamefanya vitendo vya dharau kwa kitabu hicho kitakatifu kwa Waislamu.

Lakini kamanda wa kituo hicho amesema kuwa hakuna ushahidi unaoaminika uliopatikana kuwa kitabu cha Koraan kilitumbukizwa chooni.

Jarida la News Week liliripoti madai ya kutumbukizwa kitabu hicho chooni mapema mwezi huu, lakini baadaye ilikana madai hayo.

Ripoti hiyo ya News Week ilizusha maandamano makubwa, yaliyosababisha vifo vya kiasi cha watu 15 nchini Afghanistan.