1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Malumbano ya maseneta

2 Novemba 2005

Seneti ya Marekani imefanya mkutano wa siri wa kudai kukamilishwa kwa uchunguzi juu ya madai ya kutumiwa vibaya kwa idara ya upelelezi na ikulu ya Mrekani katika kuhalalisha sababu ya kuanzisha vita ya Iraq.

Wabunge wa chama cha Democtrat walitumia nafasi hiyo kuwalazimisha wanasheria kujadili swala hilo lakini wenzao wa chama cha Republican wameielezea hatua ya wabunge wa Democrats kama tamthilia.

Hata hivyo wabunge wa Republicans wamekubali kuunda tume ya vyama vyote viwili itakayo toa taarifa juu ya kamati ya upelelezi inavyo endelea na uchunguzi wake kufikia Novemba 14.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW