1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington: Mapinduzi baridi yasifiwa

24 Novemba 2003

Mageuzi ya amani ya uongozi nchini Georgia yamekaribishwa kwa mikono miwili. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani, Colin Powell, amemhakikishia Kaimu Rais Burdshanadse msaada wenye lengo la kuimarisha demokrasia na mageuzi ya serikali nchini Georgia kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo. Wakati huo huo, serikali ya Marekani imemshukuru Shevardnadse kwa kuifanya Georgia kuwa miongoni mwa jamii ya kimataifa. Mkuu wa mambo ya nchi za nje wa Umoja wa Ulaya, Javier Solana, amesema katika Runinga ya Ujerumani kuwa yaliyotokea Georgia yamefanywa kwa busara kubwa na kuzuia kila aina ya utumiaji wa nguvu. Serikali ya Ujerumani imetangaza kuwa iwapo Shervardnadse ataamua kuondoka Georgia anakaribishwa Ujerumani kwa sababu amesaidia sana muungano wa Ujerumani alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Urussi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW