Washington: Marakeni yatafuta uelewano pamoja na washirika
13 Novemba 2003Matangazo
Ugunduzi wa Shirika la uchunguzi la Umoja wa Mataifa, kwamba hakuna ushahidi kuwa Iran ina mpango wa silaha za kinyuklia "huwezi kamwe kuaminika," alisema hiyo jana naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Bolton. Katika jibu la kwanza rasmi la Marekani, kuhusu ripoti ya Shirika la Nishati ya Atomiki Duniani, Bolton alisema ripoti hiyo kwa hakika inahakikisha maoni ya Marekani, kwamba juhudi kubwa za Iran juu ya kujipatia uwezo tete wa kinyuklia zinamaanisha tu kuwa ni sehemu ya mpango wa silaha za nyuklia.
