1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington: Marekani inaitaka Serbia iwakabidhi Radovan Karadjic na Ratko Mladic kwa Mahakama ya The Hague

12 Julai 2005

Marekani imeitaka tena Jamhuri ya Serbia iwakabidhi Radovan Karadzic na Ratko Mladic, watu wanaoshukiwa kuendesha uhalifu wa kivita katika Bosnia, mbele ya mahakama ya uhalifu wa kivita ilioko The Hague. Rais George Bush wa Marekani, alisema: katika kuukumbuka mwaka wa kumi tangu kufanyika mauaji ya Srebrenica, huu ni wakati wa kujikumbusha kwamba kuna watu waliowauwa bila ya huruma na bila ya kujali watu wasiokuwa na hatia. Jana maelfu ya watu katika mji wa Srebrenica waliwakumbuka Waislamu 8,000 waliouliwa katika mji huo na majeshi ya Wa-Serbia wakati wa Vita vya Bosnia, licha ya kwamba mji huo ulikuwa chini ya ulinzi wa majeshi ya usalama ya Umoja wa Mataifa. Wawakilishi wengi wa kimataifa wameelezea masikitiko yao kwamba jamii ya kimataifa hayajayazuwia mauaji hayo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW