WASHINGTON: Marekani kuendelea kuichukulia vikwazo Libia
6 Januari 2004Matangazo
Rais George W Bush wa Marekani, amesema Marekani itaendelea kutekeleza vikwazo vilivyochukuliwa Libia na nchi yake, licha ya matamshi ya hivi majuzi ya wakuu wa Libia, kwamba wameamua kuachana na miradi yote inayohusika na mitambo na silaha za kinuklia. Katika barua aliyowaandikia wabunge wa nchi yake hata hivo, Rais George W Bush anasema ikiwa Libia itaendelea na sera ilizotangaza siku chache zilizopita, basi Marekani itafikiria pia vipi kuregeza msimamo wake.
Duru za kidiplomasia mjini Washington, zinasema uamuzi huo wa Rais wa Marekani haujamshangaza yeyote, licha ya kampeni iliyokuwa ikiendeshwa na wakuu wa Libia.
Wiki iliyopita, Waziri mkuu wa Libia Chokri Ghanem, aliliambia gazeti la Marekani New York Times, kwamba ikiwa Marekani haitafuta vikwazo ilivyowekea nchi yake, basi Libia huenda haitalipa pesa zilizosalia, za fidia ya familia za wahanga wa kulipuliwa ndege ya shirika la Marekani PanAm, Lockerbie-uskochi; mwaka wa 1988.
Akasema Marekani inastahiki kuizawadia Libia kuondolewa vikwazo hivyo, ili kuyaruhusu Mashirika ya Marekani ya biashara ya Petroli, kurejea Libia.