WASHINGTON: Marekani kuisaidia Uturuki kupambana na PKK
6 Novemba 2007Matangazo
Rais wa Marekani George W.Bush ameahidi kumsaidia Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kupambana na waasi wa Kikurd.Amesema,waasi wa Kikurd wa chama cha PKK kilichopigwa marufuku,ni adui wa wote-Uturuki,Irak na Marekani.Bush alitamka hayo baada ya kukutana na Erdogan mjini Washington.Mada kuu ya majadiliano yao ilihusika na kitisho cha Ankara kuwa itawashambulia waasi wa Kikurd kaskazini mwa Irak.
Bush amesema,Marekani itashirikiana na Uturuki kubadilishana habari za upelelezi katika juhudi ya kuzuia mashambulizi hayo.Marekani ina hofu kuwa mashambulizi ya Uturuki kaskazini mwa Irak yatachafua eneo lenye utulivu wa aina fulani.